Tanzania yaachana na kocha Amunike

Emmanuel Ammunike pengine ndio jina lililotajwa zaidi ndani ya mwezi mmoja mpaka sasa, kwa wadau wa soka nchini Tanzania. Kila mmoja amekuwa akilitaja jina hilo kwa namna na sababu tofauti. Lakini kubwa zaidi ni namna ya kufuzu na matokeo ya michezo ya Afcon 2019.

Sasa baada ya kutajwa zaidi jina hilo, leo imetoka taarifa rasmi ya kukata mzizi wa fitina kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kusitisha kandarasi ya Amunike katika kukinoa kikosi cha Taifa Stars.

Kupitia taarifa rasmi iliyotumwa na TFF kwa vyombo vya Habari leo Julai 8, 2019 imethibitisha, imeandikwa kama ifuatavyo:-

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Timu ya Taifa “Taifa Stars” Emmanuel Amunike tumefikia makubaliano ya pamoja kusitisha mkataba baina yetu.

TFF itatangaza Kocha wa muda atakaekiongoza Kikosi cha Timu ya Taifa kwa mechi za CHAN.

Akichukua mikoba ya Salum Mayanga, Emmanuel Amunike aliajiriwa Mwezi August 7, 2018 kwa kandarasi ya miaka miwili kukinoa kikosi cha Taifa Stars pamoja kufundisha vikosi vya timu za Taifa kwa vijana wenye umri wa miaka 23, 20, na 17.

MAFANIKIO YA AMUNIKE NA STARS

Kwa miezi aliyokaa Tanzania Amunike amefanikiwa kuifikisha Tanzania Afcon 2019 nchini Misri kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments