Bale atamba wakati Real Madrid ikiibwaga Celta Vigo

Tangu mwaka 2013 Barcelona haijawahi kupoteza mchezo wowote kwa Athletic Bilbao lakini katika mchezo wa ufunguzi mabingwa wa La Liga wamepoteza mchezo huo kwa goli 1-0.

Jumamosi sasa, Real Madrid baada ya kupitia mabonde kwenye maandalizi ya msimu huu kuanzia kwa kocha na wachezaji hata uongozi sasa licha ya mabonde hayo Madrid wameanza kwa ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Celta Vigo.

Katika hali isiyo ya kawaida kocha Zinedine Zidane alianza mchezo huo kwa kumuanzisha Gareth Bale amesaidia goli moja kwenye ushindi huo.

Valencia wametoshana nguvu na Real Sociedad kwa sare ya goli 1-1.

Real Mallorca wameibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Eibar katika mchezo uliopigwa leo Jumamosi.

Leganes wamefungwa moja kwa bila na Osasusana.

Goli 8 zimefungwa ndani ya dakika tisini katika mchezo wa Villarreal dhidi ya Granada ambapo mpaka kipenga cha mwamuzi cha matokeo yalikuwa 4-4.

Kwa matokeo hayo, Real Madrid wanaongoza kwa muda kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania La Liga.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends