Man United, Liverpool zasonga mbele Carabao Cup

202

Mechi mbili zilizovuta hisia za wapenzi wa mpira wa miguu kote duniani zimemalizika huku kila timu ikivuna ilichopada katika mchuano wa Kombe la Carabao uliochezwa Jumatano hii.

Staa wa Manchester United Marcus  Rashford, ameibuka shujaa baada ya kufunga goli mbili katika ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Chelsea dimba la Stamford Bridge. Mabao hayo yanaifanya United kufuzu hatua ya robo fainali ya mchuano huo wa leo wakati ambao goli la Chelsea likifungwa na Mitch Batshuayi akimzidi ujanja Harry Maguire.

Rashford alianza kucheka na nyavu dakika ya 23 kwa penalti kabla ya Mitch Batshuayi kusawazisha dakika ya 61 na bao la ushindi  kwa United likafungwa dakika ya 73 kwa mpira uliokufa uliozama mazima nyavuni ulipigwa na Rashford uwanja wa Stamford Bridge. Dimba la Anfield, Arsenal ilisafiri mpaka jiji la Liverpool kumenyana vikali dhidi ya Liverpool ambalo mchezo umetamatika kwa sare ya 5-5 kabla matuta hajaamua mchezo huo.

Hatua ya matuta Liverpool waliokuwa wenyeji wa mchezo huo kushinda enati tano na Arsenal tatu. Wapigaji kwa upande wa Arsenal ni Bellerin, Guenduozi, Martinell hawa walipata, Ceballos alikosa, Maitland- Niles alipata.

Kwa upande wa Liverpool alianza Milner, Lallana,Brewster Origi na Jones alimaliza kwa kufunga penalti ya ushindi. Baada ya timu zote kufuzu kwa ajili robo fainali, mchakato wa droo umepangwa kufanyika siku ya Alhamis.

Author: Asifiwe Mbembela