Napoli yaiduwaza Juventus, Maurizio Sarri akalia kuti kavu Turin

373

Napoli wametangazwa kuwa mabingwa wapya wa Coppa Italia baada ya kuwachabanga Juventus kwa penati 4-2 katika mchezo uliopigwa Jana Jumatano katika dimba la Stadio Olimpico kufuatia sare tasa kwenye dakika 90.

Penati ya Arkadiusz Milik iliipa ubingwa Napoli baada ya miaka sita bila kushinda taji lolote kubwa kama hilo, kiungo mshambuliaji wa Juventus Paulo Dybala na mlinzi wa pembeni wa timu hiyo Danilo walikosa matuta upande wa Juventus.

Penati ya kwanza ya Napoli alipiga Insigne, Matteo Politano na Maksimovic zote zilikwama nyavuni wakati Milik pekee alisubiliwa kutamatisha mafanikio ya Napoli na alifanya hivyo.

Mbali na kuwa taji la kwanza kwa Napoli baada ya miaka sita, lakini pia ni ubingwa wa kwanza kwa kocha mtukutu wa Napoli Gennaro Gattuso, hata hivyo kocha wa sasa wa Juventus Maurizio Sarri atakuwa amekalia kuti kavu kwa kukosa taji la Coppa Italia mara mbili mfululizo.

Author: Bruce Amani