Arsenal yaanza Europa League kwa kishindo

Arsenal imeifunga timu ya Ukraine ya Vorskla Poltava mabao 4-2 katika mechi ya kwanza ya ligi ya Ulaya, Europa League. Mabao mawili yamefungwa na mshambuliaji wa timu ya Uingereza ya Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gabon. Mabao mengine mawili yamefungwa na kiungo wa timu hiyo Mesut Özil pamoja na mchezaji wa mbele, Danny Welbeck. Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, timu ya RB Leipzig ya Ujerumani imefungwa mabao 3-2 na klabu ya Austria ya Red Bull Salzburg huku Eintracht Frankfurt pia ya hapa Ujerumani, ikiilaza Marseiile ya Ufaransa kwa magoli 2-1.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends