Man City yaifunga Arsenal 1-0, na kutawala kileleni mwa EPL

Manchester City imefikisha mechi 18 za ushindi mfululizo kufuatia kuondoka na alama tatu katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa Leo Jumapili dhidi ya Arsenal kwa kushinda bao 1-0.

Man City ambao walikuwa wageni kwenye dimba la Emirates hawajapoteza mchezo wowote tangia Disemba 15, waliweza kupata goli la kuongoza ambalo limeibuka kama goli la mchezo huo kupitia kwa Raheem Sterling akimalizia kwa kichwa krosi ya Riyard Mahrez ungwe ya kwanza.

Matokeo hayo yanaifanya City kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa EPL kwa tofauti ya alama 10 huku michezo 13 pekee ikiwa imesalia.

Arsenal wanakamata nafasi ya 10 alama sita kuingia nne bora.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares