Namungo FC yaitandika 6-2 timu kutoka Angola ya Clube Desportivo de Agosto

Timu ya Namungo leo imeibuka na ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya wapinzani wao Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa kufuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, Namungo ilikuwa ya kwanza kufungwa bao kabla ya kusawazisha bao hilo na kupata mabao mengine na mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya kuashiria kumalizika kwa mpira huo, Namungo aliibuka na ushindi wa mabao 6-2.

Wafungaji wa mabao katika mchezo huo ni kama ifuatavyo kwa upande wa Namungo ambao walikuwa wageni kwenye mechi hiyo kikanuni licha ya kucheza nyumbani Hashimu Manyanya, Sistus Sabilo goli mbili, Leriant Lusajo, Kwizera na Stephen Sey.

Mtanange wa marudiano utachezwa masaa 72 baada ya mchezo wa awali kwa mujibu wa CAF kwa maana hiyo Jumatano hii ya Februari 25 kutakuwa na kipetu tena.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares