Al Ahly yawafundisha kandanda Vita Club Ligi ya Mabingwa

Kikosi cha kocha Pitso Mosimane cha Al Ahly kimeitandika AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa bao 3-0 mtanange uliopigwa dimba la Stade des Martyrs Leo Jumanne Machi 16.

Mtanange uliopita baina ya timu hizo ulilala kwa sare ya goli 2-2 kwa maana ya timu zote mbili kufikisha alama nne katika mechi tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo uliokuwa umeruhusiwa mashabiki 3,000, magoli ya Ahly yamefungwa na Mohamed Sherif, Mohamed Magdi Afsha kipindi cha kwanza na Mohamed Taher aliweka kimiani kwa bao la dakika ya tatu.

Al Ahly wanafikisha mechi nne alama saba bado kuna mechi mbili za kuhitimisha kundi A ambapo klabu mbili zenye alama nyingi zaidi zitasonga mbele kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi hiyo.

Kwa sasa msimamo umekaa hivi: Simba (10), Al Ahly (7), Vita Club (5) na Al-Merrikh (1).

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends