Jezi Mpya Yanga zatambulishwa, Manara atia neno

Klabu ya Yanga imetambulisha rasmi jezi mpya za msimu mpya wa mashindano 2021/22 zikizinduliwa na mmoja wa wasemaji wa klabu hiyo Haji Sunday Manara baada ya kutambulishwa siku moja akitoka kwa wapinzani wao klabu Simba.

Uzi huo wa aina tatu, nyumbani, ugenini na nyingine ya tatu zenye rangi ya njano na kijani wanakusudia kuzitumia jezi hizo kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa kirafiki kwenye kileleni mwa Wiki ya Mwananchi Agosti 29 Jumapili.
Akitambulisha jezi hizo, Haji Manara amesema wale wote wenye shaka juu ya uwezo wa kufanya kazi kwa wafanyakazi wa nafasi hiyo akiwemo Hassan Bumbuli na Antony Nugaz, Manara amesema atafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wote wawili.
Amesema baada ya kutambulishwa kumekuwa na mijadala mingi watu wakihoji ndugu zake Nugas na Bumbuli watafanya kazi gani.
“Nimekuja Yanga kufanya kazi niwahakikishie Bumbuli na ndugu yangu Nugaz mtafurahi kufanya kazi na mimi kuweni na amani tupo pamoja,” anasema na kuongeza kuwa.
“Hawa ni ndugu zangu nawafahamu sana hivyo tutaungana pamoja kufanya kazi bora ndani ya Yanga tutahakikisha inakuwa bora kila idara,” anasema.
Kila mmoja amekuwa akisema yake kwenye utambulisho huo pamoja na Manara kuwepo kwenye klabu ya Yanga.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares