Liverpool, Chelsea zatoshana nguvu EPL

Mchezo wa aina yake, ukamalizika kwa utata mkubwa lakini wenye kutoa nishani kwa kila timu. Chelsea wakimaliza dakika 90 pungufu kufuatia Reece James kuonyeshwa kadi nyekundu wakati Kai Havertz akitangulia kuipatia goli The Blues.

Mchezo huo ukipigwa dimba la Anfield mbele ya mashabiki lukuki, walijikuta wako nyuma kwa bao la Kai, hata hivyo Liverpool ambao ni mabingwa wa Ligi msimu juzi walirudisha bao hilo kwa mkwaju wa penati ya Mohamed Salah.

Sare ambayo kwa Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Chelsea itakuwa na uafadhali hasa kutokana kucheza muda mwingi wakiwa pungufu.

Matokeo hayo yanaifanya Chelsea kufikisha alama saba sawa na Majogoo wa Jiji la Merseyside Liverpool wenye alama saba, upande mwingine Virgil van Dijk ameendelea kuimarika kufuatia kuwa nje takribani mwaka mzima kutokana na majeruhi

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares