
Vigogo kuangushana katika Champions League
Vigogo vya soka vingi katika barani la Ulaya vinahitaji pointi moja tu kujihakikishia kuingia katika duru ya mtoano, lakini mbinyo wa Champions League unaikabili zaidi Paris Saint-Germain na Tottenham, wakati Bayern Munich ikihitaji kwa udi na uvumba msukumo zaidi.
Vigogo vingi vitakuwa na matumaini kesho Jumanne na kesho kutwa Jumatano kujiunga na Barcelona katika timu 16 zinazobakia katika Champions League, wakati nyingine zikitaraji kuepuka kuondolewa.
Mabingwa wa Ulaya Real Madrid, Manchester City, Bayern Munich, Roma, Juventus, Inter Milan na Porto zote zinahitaji pointi moja katika awamu hii ya makundi kufuzu.
Baadhi ya timu nyingine zitakuwa na matumaini ya kukata tikiti zao kwa ushindi, wakati timu kama Paris Saint-Germain, Tottenham Hotspur na Valencia zinapambana na hali zao.
Kundi C ni moja kati ya makundi ambayo timu zinakaribiana sana ambako Napoli itafuzu iwapo itaishinda Red Star Belgrade na PSG itashindwa kuiangusha Liverpool.
Hiyo ndio hali ya mambo katika kinyang’anyiro hicho ambapo kikosi cha Juergen Klopp kinatarji kukamilisha hatua hiyo kwa ushindi mjini Paris iwapo Napoli itaepuka kushindwa, lakini PSG, ambayo inamatumaini ya kuongezewa nguvu na wachezaji wake wa kati Neymar na mshambuliaji Kylian Mbappe, watakuwa wakipigania maisha yao
