Real yakamata nafasi ya tano baada ya kuishinda Valencia

180

Real Madrid imekwea mpaka nafasi ya tano nyuma ya vinara Sevilla baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Valencia katika mchezo uliofanyika katika dimba la Bernabeu.

Iliwachukua dakika ya 19 Madrid kuwa kifua mbele kupitia kwa goli la kujifunga la Daniel Wass kabla ya shuti kali lilopigwa na Lucas Vazquez kutinga wavuni. Umekuwa ushindi wa sita kwa Santiago Solari katika michezo saba alioinoa timu hiyo tangu mwezi Oktoba.

Shuti kali la Gareth Bale lilikataliwa na mlinda mlango Neto na Karim Benzema likipaa juu mwanzoni mwa mchezo huo.

Valencia ilipata nafasi moja ya wazi kupitia kwa Santi Mina ambaye aliachia kombora kali hatua 10 nje ya kisanduku.

Matokeo hayo yanaifanya Valencia kusalia nafasi ya 13 katika ligi ya kandanda ya Hispania, ambapo Real Madrid imepanda nafasi ya tano sawa na Alaves zote zikiwa na alama 23 ambapo timu zote tatu zimecheza leo Jumapili.

Author: Bruce Amani