Napoli yapumua nyuma ya Juventus

243

Napoli imeikandamiza bila huruma Frosinone 4-0 katika mchezo wa Serie A matokeo yaliyoifanya kuwa alama nane nyuma ya vinara Juventus huku wakiwa katika nafasi nzuri ya kuendelea kuifukuzia Juventus.

Juventus iliendeleza ubabe dhidi ya Inter Milan, baada ya kuitwanga Milan goli 1-0 na sasa imefikisha alama 43 katika michezo 15 ambapo haijapoteza mchezo hata mmoja.

Piotr Zielinski na Adam Ounas walijaribu kupiga mashuti ya mbali mara kadhaa kabla ya shuti la Kipindi cha pili la Arkadiusz Milik katika dimba la San Paolo kutinga wavuni.

AS Roma ililazimishwa sare ya goli 2-2 dhidi ya Cagliari, goli la pili katika dakika za lala salama ikiwa nyuma wachezaji wawili liliiwezesha Cagliari kupata sare hiyo.

Roma ilipata uongozi kupitia kwa Bryan Cristante na Aleksandar Kolarov kwa njia ya faulo.

Artur Ionita alifunga goli la kwanza upande wa Cagliari dakika sita kabla mchezo kumalizika huku mlinzi Darijo Snra na Luca Ceppiteli kutolewa nje kwa kadi nyekundu hata hivyo haikuwazuia wabishi Cagliari kupata alama moja baada ya Marco Sau kusawazisha. Sare hiyo imeifanya Cagliari kukamata nafasi ya 13. Roma ilipanda hadi nafasi ya sita alama nne juu ya watani wa jadi Lazio, ambao nao walitoka sare ya goli 2-2 dhidi ya Sampdoria.

Lazio ilikuwa inaongoza kwa goli 2-1 baada ya penati iliyoamuliwa na mwamuzi kwa njia ya VAR  ingawa Riccardo Saponara aliweza kusawazisha dakika tisa kabla mchezo haujamalizika.

Sampdoria ilikuwa inaongoza Kipindi cha kwanza baada ya goli la mkongwe Fabio Quaqliarella lake la nane la msimu kabla ya mlinzi Francesco Acerbi kusawazisha katika dakika ya 79 ya mchezo.

Immobile amefikisha goli 10 katika Serie A sawa na mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo na straika wa Genoa Krzystof Piatek.

Lazio sasa wako tofauti ya magoli na AC Milan ambayo imekaa nafasi ya nne nyuma ya Inter Milan ambayo ina mchezo Jumapili 8 Disemba dhidi ya Torino walioko nafasi ya kumi na nane.

Author: Bruce Amani