Abidal ashinda vita ya Messi

Mkurugenzi wa michezo Barcelona Eric Abidal ataendelea kushikilia kiti chake cha uongozi klabuni hapo licha ya kukosolewa na supastaa Lionel Messi kwa kile alichoeleza kuwa wachezaji walishindwa kujitolea vema kipindi Barca inanolewa na Ernesto Valverde.

Mshindi huyo mara sita wa Ballon d’Or Messi alipinga wazi wazi kauli iliyotolewa na Abidal baada ya kusema chini ya Valverde miongoni mwa wachezaji hawa kuonyesha nia ya dhati kujituma kwa ajili ya timu.

Itakumbukwa kuwa Valverde alifukuzwa mwezi Januari na nafasi yake ikachukuliwa na Quique Setien.

Barcelona iliitisha kikao cha dharura kilichohusisha viongozi wa juu wa klabu sambamba na Abidal na Lionel Messi ili kutuliza hali ya hewa ya klabu hiyo, baada ya kikao hicho kilichochukua takribani masaa mawili siku ya Jumatano waliamua kulimaliza jambo hilo kwa pamoja.

Pamoja na kulimaliza jambo hilo, Barcelona iliamua mchezaji huyo za zamani wa Ufaransa ataendelea kuhudumu kama Mkurugenzi wa michezo ndani ya FC Barcelona.

Abidal, ambaye ni mchezaji mweza wa Messi 2007-13 aliyasema hayo katika mahojiano na kituo cha Diario Sport cha nchini Hispania ambapo muda mfupi baada ya mahojiano hayo, Lionel Messi aliibuka na kuandika kuwa “Unapozungumzia wachezaji tuko wengi, hivyo inatakiwa utaje na majina ya wachezaji ambao unaona walikuwa hawajitumi kuliko kuongea vitu usivyo na uhakika nao”.

“Kila mmoja anatakiwa kuwajibika katika nafasi yake lakini tukiruhusu kuingilia katika majukumu haipendezi”.

Yote hayo huenda yakaendelea kuiandama Barcelona kwani licha ya kumtimua Valverde bado haifanyi vizuri kwani wakati anaondoka Ernesto Barca ilikuwa kinara wa La Liga lakini sasa inakamata nafasi ya pili.

Pili, Messi aliamua kuibuka na kuyasema hayo ni baada ya kujihisi ananyoshewa kidole yeye kwani tangu mwanzoni wa msimu huu aliiomba klabu kumrudisha Neymar sambamba na kusajili mshambuliaji lakini Barcelona haikutimiza hata moja- Guillem Balague

Author: Bruce Amani

Facebook Comments