African Sports yaibania Simba kweupe mchezo wa kujipima nguvu

Simba SC imetoshana nguvu na African Sports kwa kutoa sare ya 0-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo Jumatatu Novemba 16 kwenye dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam majira ya saa moja usiku.

Simba ambayo inakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 20 ilishindwa kuifumua safu ya ulinzi ya African Sports ambayo imecheza vizuri kwa asilimia kubwa ya dakika za mchezo huo.
Wakati huo huo African Sports ambao wanashiriki Ligi daraja la kwanza wakitumia mkoko mzima tofauti na Simba ambao baadhi ya nyota wake wako kwenye majukumu ya timu ya taifa.
Kikosi cha Simba ambacho kilianza kwenye mtanange wa leo ni Ally Salim, Henry Hussein, Hassan Mohammed, Kennedy Juma, Ibrahim Ame, Rally Bwalya, Clatous Chama, Ibrahim Ajibu, Charles Ilafyia, Fransis Kahata na Miraji Athumani.

Author: Asifiwe Mbembela