Aguero akumbwa na majeruhi tena, kuwa nje kwa karibu mwezi mmoja

91

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Kun Aguero atakosa mechi ya ugenini ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Marseille leo Jumanne kutokana na majeruhi.

Aguero, 32, ambaye alikuwa majeruhi kabla ya kurejea na kucheza mechi tatu pekee alipata majeruhi mengine katika mchezo wa Ligi dhidi ya West Ham United,  na atakuwa nje kwa muda wa takribani siku 30 akiuguza majeruhi yake.

Beki wa kati Aymeric Laporte amesafiri na timu kwenda Ufaransa kucheza mechi ya pili ya Uefa kundi C lakini pia huenda kiungo mshambuliaji Kelvin de Bruyne akacheza mechi hiyo kufuatia kucheza mechi ya wikiendi.

Hata hivyo, Fernandinho, Benjamin Mendy na Nathan Ake watakuwa nje ya dimba.

Author: Bruce Amani