Aguero akutwa na majeruhi tena

144
Mshambuliaji wa Barcelona Sergio Aguero analazimika kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki 10 kufuatia kupata majeruhi wakati wa maandalizi ya msimu ujao 2021/22.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga imesema kuwa Aguero aliyejiunga na klabu kutokea Man City atakuwa nje kwa  muda huo au zaidi baada ya vipimo.
Aguero, 33, alijiunga na Barcelona kutokea Manchester City kwa mkataba wa miaka miwili kuanzia mwezi Juni. Alitumia miaka 10 Manchester City ambapo kwa kipindi hicho alifunga goli 260 kwenye mechi 390.

Author: Bruce Amani