Ajax yakaribia kumsajili Sebastien Haller wa West Ham United

310

Mshambuliaji ghali wa West Ham Sebastien Haller yuko mbioni kukamilisha uhamisho wake na kutua katika klabu ya Ajax. Wagonga Nyundo wa London walitumia pauni milioni 45 kumsajili strika huyo raia wa Ivory Coast mwaka 2019 chini ya kocha Manuel Pellegrini lakini hakufanya vizuri kama ambavyo ilikusudiwa awali.

Pellegrini alifutwa kazi ya ukocha Disemba 2019 na timu kuchukuliwa na David Moyes ambaye mpaka sasa yupo klabuni hapo.

Licha ya hela kubwa iliyotumika kumnunua Haller, klabu ya West Ham iko tayari kumuuza kwa bei ya hasara ya pauni milioni 22.5

Author: Asifiwe Mbembela