Al Ahli Tripoli yapewa pointi za mezani dhidi ya Biashara United ya Tanzania

Katika hali isiyokuwa ya kawaida katika karne ya 21, yenye utandawazi maendeleo makubwa katika nyanja tofauti, kikosi cha Biashara United ya Mara kimeshindwa kusafiri kuelekea Libya kwenye mechi ya mkondo wa pili kuwania kufuzu nafasi ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Biashara United ilikuwa inatakiwa kusafiri kabla ya Leo Jumamosi kwenda huko Libya kumenyana vikali na Al Ahli Tripoli huku wakiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 2-0 nyumbani lakini wameshindwa kutokana na sababu mbalimbali kubwa ambayo inaatajwa ni uhaba wa fedha.

Pamoja na jitihada za Shirikisho la Kandanda Tanzania TFF kupambana kuona uwezekano wa kuusogeza mchezo mbele, hatua hiyo haijafanikiwa na timu ya Al Ahli Tripoli imepewa ushindi wa goli tatu na alama tatu.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends