Al Ahly watwaa ndoo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, yaichapa 3-0 Kaizer Chiefs

Klabu ya Al Ahly imeibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mtanange uliopigwa nchini Morroco Jumamosi ya Julai 17 na kutwaa ubingwa wa Caf mara ya 10.

 

Al Ahly ambao wana kocha raia wa Afrika Kusini na shabiki wa zamani wa Kaizer Chiefs Pitso Mosimane walitangulia kujipatia bao kupitia kwa Mohamed Sherif kabla ya kutengeneza bao lingine, akiwa nyota wa mchezo.

 

Ahly walipata upenyo mwepesi wa kutawala kabumbu ndani ya dakika 45 za ungwe ya pili kufuatia Happy Mashiane wa Chiefs kuonyeshwa kadi nyekundu.

 

Kadi hiyo iliruhusu mshambulizi kutokea ya mara kwa mara ambapo Mohamed ‘Afsha’ Magdy alifunga bao la pili na baadaye Amr El Solia kuongeza lingine likiwa la kuhitimisha karamu ya magoli kwa Al Ahly ambao wameendelea kujitengenezea historia ya kipekee barani Afrika.

 

Ubingwa huo unakuwa wa 10 kwa Ahly ambao sasa wameipita Zamalek ya Misri na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa tofauti ya mataji matano kwa wote wawili wameshinda kila mmoja mara 5.

 

Kocha Mosimane wa Al Ahly ameandikisha rekodi ya kushinda taji hilo, kumbuka Ahly ni mara ya pili mfululizo lakini kwake alitangulia kushinda msimu wa 2016 alipokuwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends