Alaba atambulishwa rasmi Real Madrid, apewa jezi nzito, akataa kulinganishwa

Mlinzi mpya wa Real Madrid David Alaba amesema kuwa hategemei kurithi mikoba ya aliyekuwa beki wa timu hiyo Sergio Ramos kufuatia kukabidhiwa jezi namba yake, namba nne mgongoni.

 

Nyota huyo wa kimataifa wa Austria Alaba, 29, alijiunga kama mchezaji huru Real Madrid kufuatia mkataba wake ndani ya Bayern Munich kumalizika mwezi Mei.

 

Ramos, aliyetumika Madrid kwa miaka 16, alijiunga na Paris St-Germain akiwa katika umri wa miaka 35 baada ya kandarasi yake kumalizika Santiago Bernabeu mwezi Juni.

 

“Kila mmoja anajua Ramos alikuwa hapa kwa muda mrefu akivaa jezi hii, na kuwa kiongozi mkubwa”, alisema Alaba baada ya kutambulishwa rasmi.

 

“Ni heshima kubwa kuvaa jezi yenye namba ya mchezaji mithili ya Ramos, itaniongezea kasi na juhudi”.

 

“Jambo la msingi siko hapa kujilinganisha na wachezaji/mchezaji mwingine, niko hapa kucheza na kujaribu kuisaidia timu kushinda mataji, Mimi ni Alaba sio mwingine”.

 

Ramos ni mchezaji mwenye mechi nyingi zaidi kutokea Hispania akiwa ameshinda Kombe la La Liga mara tano, ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara nne.

 

Alaba, amemwaga wino wa miaka mitano, akiwa Bayern alishinda mataji 10 ya Bundesliga, 2 Ligi ya Mabingwa na Kombe la Ujerumani mara sita akiwa na mtoto aliyekuzwa mazingira ya Allianz Arena.

 

Kiraka huyo atakuwa chini ya kocha wa zamani wa Everton Carlo Ancelotti kufuatia kuondoka klabuni hapo kwa kocha Zinedine Zidane.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares