Algeria kumenyana na Guinea kuwinda robo fainali

Algeria inaingia uwanjani leo Jumapili saa 4 usiku dhidi ya Guinea. Inaingia kwa umakini mkubwa wa kujiuliza wapi Morocco na Misri wamejikwaa baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya mwaka huu mapema.
Algeria inakutana na Guinea katika mchezo wa hatua ya 16 bora kutafuta nafasi ya kuingia hatua ya robo fainali. Huku timu zote zikiwa hazina kiwango bora sana kulingana na matokeo ya hatua ya makundi.
Timu hizi mbili zimekutana mara mbili kabla ya mtanange wa leo kwenye mashindano ya Afcon, huku mtanange wa 1980 nchini  Nigeria, Algeria ilishinda goli 3-1 wakati mwaka 1998 Burkina Faso Guinea ilishinda 1-0. Huu utakuwa mchezo wa tatu, nani kuibuka na ushindi.
Mshindi wa mchezo huu atakutana na timu ya Mali au Ivory Coast.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments