Algeria yaitwanga Guinea bila huruma na kuingia robo fainali

Riyad Mahrez ameipeleka robo fainali timu yake ya Algeria baada ya kuongoza kikosi hicho kuinyuka Guinea goli 3-0 katika mashindano ya Afcon 2019 yanayoendelea nchini Misri mtanange uliofanyika dimba la Alexandria.

Algeria watakutana na Mali au Ivory Coast robo fainali ya michuano hiyo siku ya Alhamis Julai 11.

Ushindi wa Algeria ulianza kuonekana kupitia goli la mapema likifungwa na Belaili katika kipindi cha kwanza, mpaka kipindi hicho kinamalizika matokeo yalikuwa bora kwa Algeria 1-0.

Sherehe ya ushindi iliendelea baada ya kuanza kipindi cha pili ambapo Youcef Atal aliongoza timu hiyo kabla ya goli nzuri la Mahrez kuhitimisha ushindi wa Algeria baada katika mchezo wa hatua ya 16 bora.

Guinea imeshindwa kuonyesha kiwango katika mchezo huo iliwachukua dakika 54 kuandika shuti moja lililolenga likipigwa na Mady Camara.

Unakuwa mchezo wa nne mfululizo kwa Algeria bila kuruhusu kuguswa kwa nyavu zao katika mashindano ya Afcon 2019 nchini Misri.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments