Algeria yatawala tuzo za wachezaji binafsi Afcon

305
Licha ya kubeba taji la pili la Afcon katika historia ya taifa, Algeria wametawala pia hata kwenye tuzo ama zawadi binafsi ya wachezaji katika vipengele mbalimbali vya mashindano hayo yaliyofikia tamati Ijumaa nchini Misri.
Kiungo wa Algeria Ismael Bennacer amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano, kiungo huyo mwenye uwezo wa kucheza kama kiungo mshambulaiji na ukabaji ameisaidia timu yake kutwaa taji baada ya zaidi ya miaka 28.
Kipa Rais M’Bolhi wa Algeria pia ameshinda tuzo ya mlinda mlango bora wa michuano ya Afcon 2019. Lakini pia kwenye mchezo wa fainali ametwaa mchezaji bora wa mechi.
Aidha, Mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo amefanikiwa kuwa mfungaji bora wa mashindano kwa kufunga goli 5.
Kinda wa Senegal Krepin Diatta, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano.
Taifa la Senegal limebeba tuzo ya timu bora kwenye kipengele cha timu yenye nidhamu na yenye mchezo wa kiungwana.

Author: Bruce Amani