Alichokisema Ole Gunnar Solskjaer baada ya kuchapwa 5-0 na Liverpool

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema ametoka mbali na timu hiyo hivyo hawezi kukataa tamaa kwa matokeo mabaya ambayo anakutana nayo hivi sasa.

Kocha Solskjaer ameyasema hayo Leo Jumapili Octoba 24 baada ya timu yake ya Manchester United kukubali kipigo kizito kutoka kwa Majogoo wa Jiji la Merseyside Liverpool cha goli 5-0 huku kabumbu la hatari likipigwa nyumbani kwake Old Trafford.
Nyota wa mchezo kwa Liverpool ameendelea kuwa ni yule yule Mohamed Salah. Salah amehusika katika mabao manne akifunga bao tatu na kusaidia bao la Naby Keita huku bao lingine likifungwa na Diogo Jota.
Solskjaer amesema “kupoteza kwa hasimu wako inakuwa siku ngumu lakini lazima maumivu tuyabebe na kusonga mbele”.
“Tumeumia pakubwa, tumeumia kiasi kwamba hatuwezi tena kuumia zaidi ya hapa, inatakiwa tuyabebe maumivu na kuendelea kusonga mbele”, alisema akizungumza baada ya mchezo huo.
“Wachezaji wanaumia, itakuwa ngumu kurudisha hali ya upambanaji lakini kuna baadhi yao wamekomaa ni rahisi kujengwa na kurejea kazini kwa ubora”.
Ushindi wa Liverpool unakuwa ushindi mkubwa zaidi ambao Liverpool wameupata katika dimba la Old Trafford katika historia.
Kinakuwa kipigo kizito zaidi kwa Manchester United tangia Octoba 1895 ambapo Liverpool walishinda bao 7-1 Anfield, kinakuwa kipigo kizito bila wao kufunga hata goli moja tangia mwaka 1995.
“Hatukuwa vizuri kama mchezaji mmoja mmoja, hauwezi kuipa Liverpool nafasi nyingi vile, lakini sisi tumewapa”.
“Kiwango kwa ujumla hakikuwa cha kuridhisha, tulipata nafasi moja tulishindwa kuitumia wao kila nafasi waliitumia vyema”.
Nahodha wa Manchester United Harry Maguire amewaomba msahama mashabiki wa timu hiyo akisema kama wachezaji wanapaswa kujitazama vyema.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends