Aliyekuwa Rais wa CECAFA Nicholas Musonye ajitosa kinyang’anyiro cha Urais wa kandanda la Kenya

Aliyekuwa katibu mkuu wa Chama cha mpira wa Miguu Kanda Kanda ya Afrika Mashariki na Kati – CECAFA Nicholas Musonye ametangaza kuwa anawania Urais wa Shirikisho la kandanda Kenya- FKF, akionekana kutoa ushindani mkali.

Wengine wanaowania kiti hicho ni pamoja na mwenyekiti wa sasa Nick Mwendwa, Rais wa zamani wa Shirikisho hilo Sam Nyamweya, Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya AFC Leopards Alex Ole Magelo, Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Vihiga Moses Akaranga, Afisa Mkuu Mtendaji wa Gor Mahia Lordvick Aduda miongoni  mwa wengine.

Uchaguzi wa awali wa FKF ulifutiliwa mbali na mahakama ya kutatua mizozo ya soka nchini Kenya huku Shirikisho la kandanda duniani FIFA likitarajiwa kutoa mwelekeo wa ni lini utakapofanywa uchaguzi wa FKF baada ya muda wa viongozi wa sasa kukamilika

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends