Allegri asema Ronaldo haondoki Juventus

105

Kocha mkuu wa Juventus Massimiliano Allegri amesema nyota wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo hataondoka klabuni hapo msimu huu baada ya mazungumzo baina ya pande mbili.

Ronaldo, 36, aliandika kwenye ukurasa wake kuwa kuhusishwa kung’oka Juve ni sawa na kumkosea heshima kama mwanadamu na mchezaji.

Akizungumzia kuelekea mtanange wa Ligi, kocha Allegri amesema nahodha wa Ureno atabakia.

“[Ronaldo] hajawai kuonyesha nia ya kuondoka klabuni hapa, ameniambia kuwa anataka kusalia”, alisema kocha huyo.

Juventus watafungua pazia la Ligi Kuu nchini Italia dhidi ya Udinese, siku ya Jumapili.

Kwa siku za karibuni, Cristiano Ronaldo amekuwa akihusishwa kujiunga na miamba ya soka la Ufaransa Paris St-Germain, Manchester City na kurejea Real Madrid ingawa yeye mwenyewe alikanusha hali kadhalika kwa kocha wa Madrid Carlo Ancelotti.

Author: Bruce Amani