Alvaro Morata ajiunga na Atletico Madrid akitokea Chelsea

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata amejiunga na klabu ya Uhispania Atletico Madrid kwa mkopo hadi mwisho wa msimu wa 2019-20. Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Chelsea akitokea Real Madrid Julai 2017 kwa kitita kikubwa cha pauni milioni 60 kwa mkataba wa miaka mitano. alicheza mechi 47 za Premier League na kuwafungia Chelsea mabao 16. Aliichezea Atletico akiwa kinda kabla ya kujiunga na Real Madrid. Uhamisho huo umekamilika baada ya Chelsea kumsaini mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain kwa mkopo.

“Morata amedhihirisha kuwa ni mfungaji hodari wa mabao katika baadhi ya ligi zenye ushindani mkali barani Ulaya,”. Morata alisema: “Nna furaha sana na najivunia kuwa hapa.”

Callum Hudson-Odoi anahusishwa na uhamisho wa Bayern

Wakati huo huo, Chelsea imemwambia Callum Hudson-Odoi kuwa hawataki kumuuza, baada ya tineja huyo kuwasilisha ombi la kutaka aruhusiwe kuondoka. Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18, na ambaye amebakisha miezi 18 kwenye mkataba wake, amekuwa akihusishwa na ripoti za kujiunga na Bayern Munich kwa kitita cha pauni milioni 35. Kocha msaidizi wa Chelsea Gianfranco Zola amesema “Tunaamini katika kile anachoweza kuifanyia klabu hii”. Msimamo wa Chelsea una maana kuwa thamani ya Hudson-Odoi huenda ikashuka wakati atakapoingia katika mwaka wake wa mwisho kwenye mkataba wake msimu ujao.

Kwa wakati huo, Chelsea pia watakuwa na winga Christian Pulisic aliyemsaini kutoka Borussia Dortmund kwa pauni milioni 58.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends