Andrew Amonde atakuwa nahodha wa kikosi cha raga cha wachezaji saba kila upande katika mechi za ubingwa wa afrika ambazo pia zitatumika kwa kufuzu katika mashindano ya Olimpiki jijini Tokyo mwaka wa 2020 jijini Johannesberg, Afrika Kusini wikendi ijayo.
Timu hiyo yenye uzoefu wa kutosha ilitangazwa na mkurugenzi wa kiufundi wa Shirikisho la Rugby nchini Kenya – KRU Paul Feeney na Jacob Ojee atahudumu kama naibu wake Amonde. Billy Odhiambo, Willy Ambaka, Nelson Oyoo na Jeff Oluoch wote wanarejea kikosini ilhali Collins Injera atasalia nje kwa ajili ya jeraha la bega Shujaa itakabiliana na Ivory Coast katika raundi ya kwanza ya mechi za ubingwa wa Afrika
