Amonde kuwapeleka Shujaa Dubai mashindano ya IRB Series

Andrew Amonde atakuwa nahodha wa kikosi cha Rugby cha Kenya kitakachoshiriki mashindano ya kimataifa ya Rugby ya wachezaji saba kila upande – 2019/20 IRB Series ambayo yanangoa nanga Dubai mwezi ujao. Wakati akitangaza kikosi cha awali, kocha Paul Feeney amemuita tena nguli Collins Injera alikuwa majeruhi, wakati nyota Jacob Ojee, Jeffrey Oluoch, na Billy Odhiambo pia wakirudi kikosini.

 

Chipukizi hatari Johnstone Olindi, Alvin Otieno na Herman Humwa pia wamo katika kikosi hicho. Orodha ya mwisho ya wachezaji 13 watakaosafiri itatolewa wiki ijayo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends