Burundi kuivaa Tanzania mechi ya U23

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 Ngorongoro Heroes leo Jumatano inashuka dimbani katika uwanja wa Prince Rwagasore majira ya saa kumi jioni kuivaa Burundi katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu AFCON kwa vijana hao wenye chini ya umri wa miaka 23.

Mchezo huo ni muhimu kwa pande zote mbili kufanya vizuri. Kwa upande wa Tanzania wamefanya mazoezi kwa siku chake kutokana na changamoto za ratiba ya kupatikana kwa wachezaji hao ambao wengi hushiriki ligi kuu na vilabu vyao.

Mkurugenzi wa mashindano katika shirikisho la kandanda Tanzania Salum Madadi amesema ana imani na vijana hao kufanya vizuri kwa sababu asilimia kubwa ya vijana hawa hupata nafasi ya kucheza kwenye vilabu vyao.

Katika majina 19 yaliyosafiri kwenda Burundi yupo mchezaji mmoja anayecheza soka la kulipwa nchini Kenya katika klabu ya Bandari FC Abdalah Hamis ambaye mara nyingi hutumika katika nafasi ya kiungo.

Sambamba na Hamis wachezaji wengine ni Metacha  Mnata, Ally Salim, Ramadhani Kabwili, Mohamed Abdallah, Kelvin Nashon, Abdalah Shaibu,Ismael Aidan, Adam Salamba, Mbaraka Yusuph, Salim Kihimbwa, Kelvin Sabato, Habibu Kiombo, Ibrahim Hamad, Dickson Job, Nickson Kibabage, Ally Ally, Ally Msengi na Ayoub Masoud.

Ili kuweka mazingira mazuri zaidi Tanzania haina budi kushinda wakati ambao hata Burundi wanahitaji matokeo mazuri pia na hapa ndipo utamu wa mchezo huu utakapo kuwepo katika siku ya leo

Author: Bruce Amani