Kocha Saintfiet alamba mkataba mnono baada ya kuipeleka Gambia Afcon 2021

Baada ya kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Gambia kufuzu Kombe la Mataifa Bingwa Afrika – Afcon 2021, kocha mkuu wa kikosi hicho Tom Saintfiet ameongezewa mkataba mpya wa miaka mitano kuanzia sasa ambapo kandarasi yake itamalizika mwanzoni mwa mwaka 2026.

Kocha Saintfiet ambaye ni raia wa Ubelgiji kabla ya kuinoa timu ya taifa ya Gambia – The Scorpions aliyoichukua mwezi Julai 2018, alifanya kazi katika maeneo tofauti barani hapa kama taifa la Malawi, timu ya taifa ya Qatar U-17, timu ya taifa ya Ethiopia na klabu ya Free State Stars FC

Nafasi hiyo ya kufuzu Afcon 2021 nchini Cameroon imepatikana baada ya kuzizidi keti timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Angola ambao walikuwa washindani wa karibu.

Author: Asifiwe Mbembela