Mashirikisho ya michezo Kenya yalalamikia ukosefu wa mpunga

Marais wa mashikrisho ya michezo nchini Kenya waliandamana na wachezji kadhaa kuelekea bungeni  kutoa malalamishi yao kwa kamati ya bunge inayosimamia michezo nchini humo kwa kukosa kupewa ufadhili na serikali.

Rais wa Shirikisho la soka – FKF Nick Mwendwa, rais wa Raga Oduor Gangla na wengine wa michezo mbali mbali walileta malalamishi yao wiki moja tu baada ya kulalamika kwamba serikali huwa haishugulikii bajeti zao za kuboresha na kukuuza vipaji mbali na kusafiri katika michezo wanapoiwakilisha nchi. Kamati hiyo itatoa rasmi ripoti yake wiki hii baada ya kumaliza kikao.

Author: Bruce Amani