Mkuu wa kandanda CAR akamatwa Ufaransa kwa uhalifu wa kivita

Maafisa nchini Ufaransa wamemkamata mwanaume anaetuhumiwa kwa uhalifu wa kivita katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, na kiongozi maarufu wa usimamizi wa kandanda nchini humo. Hayo yamethibitishwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ikisema itampeleka mjini The Hague.

Waendesha mashtaka wamesema Patrcie-Edourd Ngaissona alikuwa kiongozi wa juu wa kundi la wanamgambo wa Anti-Balaka lililofanya mashambulizi ya kupanga dhidi ya Waislamu katika ya mwaka 2013 na 14.

Ngaissona, amabye anakanusha kufanya makosa, alichaguliwa mwezi Februari kwenye kamati ya utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu la Afrika –CAF licha ya pingamizi kutoka kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu ikiwemo Human Rights Watch.

Shirika hilo lilimtaja kama kiongozi wa Anti-Balaka katika ripoti yake ya mwaka 2016. ICC imesema Ngaissona anatuhumiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ikiwa ni pamoja na mauaji, ukandamizaji, mateso, kuwashambulia raia na kuwasajili watoto kuwa wanajeshi.

Author: Bruce Amani