Mwendwa kuwania wadhifa wa FIFA

Rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya, FKF Nick Mwendwa atawania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka duniani Fifa baadaye mwezi huu akiwakilisha kanda ya nchi zinazozungumza lugha ya kiingereza. Awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka nchini Ghana, Kwesi Nyantakyi ambaye alijiuzulu kwa tuhuma za rushwa. Sasa Mwendwa atachuana na Danny Jordan, Walter Nyamilandu, Leodgar Tenga na Elvis Chetty wa Ushelisheli.

Author: Bruce Amani