Antony Aipa Ushindi Manchester United Mbele ya Nottingham Forest

100

Manchester United imerejea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England kufuatia kutoa kichapo cha bao 2-0 dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo uliochezwa uwanja wa Forest Jumapili.

Mabao ya Manchester United yamefungwa na Antony akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Nottingham Keylor Navas baada ya shuti la Anthony Martial.

Kipindi cha pili Manchester waliendelea kutawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la pili kupitia pasi maridadi ya Antony goli likifungwa na Diogo Dalot.

Matokeo hayo yanaifanya Man United kukwea mpaka nafasi ya tatu alama tatu dhidi ya Newcastle United alama sita dhidi ya Tottenham Hotspur ambao wako nafasi ya tano.

Nottingham Forest wanashika nafasi ya 17.

Author: Bruce Amani