Tanzania yasimamisha michezo yote kutokana na COVID-19

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa wanasitisha masuala yote yanayohusu mikusanyiko ya watu isiyo ya lazima ikiwa ni kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Majaliwa amesema:-“Tumesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu kama vile Ligi Kuu ya Tanzania, Ligi Daraja la Pili, Ligi Daraja la Kwanza, lakini pia michezo ya shule za msingi (Umitashumta), michezo ya shule za Sekondari (Umiseta) pamoja na ile ya mashirika ya umma. Michezo yote hiyo imesitishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja(30) kuanzia leo.

“Kwa hiyo Wizara ya Habari na Utamaduni na Michezo yenyewe itawaandikia mashirikisho yake yote ya michezo ili kuwaambia kwamba kwa kipindi cha mwezi mmoja hiki watatakiwa kusimamisha ratiba hizo katika michezo inayochezwa kipindi hiki.”

 

Tanzania inaungana na nchi nyingine Afrika ambazo zimesitisha kuendelea kwa michezo yote miongoni mwa Kenya, Rwanda, Afrika Kusini na Morroco.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends