Arajiga Kuamua Mchezo wa Yanga, Simba Mwanza

41

Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania limemtangaza refarii Ahmed Arajiga kuwa mwamuzi wa dakika za kibabe za dabi ya Kariokoo baina ya Yanga na Simba mchezo wa nusu fainali ya Kombe la ASFC ambao utachezwa dimba la CCM Kirumba Mwanza, Jumamosi Mei 28.

Arajiga mwenye beji wa Fifa linakuwa si jambo la ajabu kwani ameshachezesha mechi kadhaa za dabi kwani hata mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita alikuwa katikati ya dimba la Benjamin Mkapa.

Pia Arajiga alikuwa katikati ya uwanja kwenye mechi ya fainali ya ASFC baina ya Simba na Yanga msimu uliopita ambapo Wekundu wa Msimbazi Simba waliibuka kidedea kwa bao 1-0 goli la Taddeo Lwanga.

Hivi karibuni refa huyo alichezesha mechi ya Ligi Kuu baina ya Geita Gold na Simba iliyochezwa katika Uwanja huohuo wa CCM Kirumba ambayo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Wakati Arajiga akipewa nafasi hiyo ya Jumamosi, marefa watatu wasaidizi ni Mohamed Mkono, Elly Sasii na Frank Komba.

Author: Asifiwe Mbembela