Argentina yagawana alama na Colombia kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022

Timu ya Taifa ya Argentina imetoka kuongoza bao mbili na mwisho wa dakika tisini wakaruhusu bao mbili huku mchezo ukimalizika kwa sare ya bao 2-2 dhidi ya Colombia waliokuwa wenyeji ukiwa ni mchezo wa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia Qatar 2022.
Baada ya mchezo huo kumalizika sasa Argentina inayoongozwa na nahodha na staa wa Barcelona Lionel Messi inaelekea kwenye michuano ya Copa America ambayo pia inaanza Jumatatu.
Bao la kuongoza kwa wageni limewekwa kimiani na Cristian Romero akitumia vyema mpira wa krosi wa Rodrigo de Paul, likiwa ni bao la kwanza kwa kijana huyo la kimataifa.
Leandro Paredes alitupia bao lingine, akitumia makosa ya walinzi pamoja na mlinda mlango David Ospina.
Colombia wakianza vyema kipindi cha pili na kupata penati ya kwanza baada ya mlinzi wa zamani wa Manchester City Nicolas Otamendi kufanya kosa kisha Luis Muriel akaingia kambani kabla ya Miguel Borja kufunga bao la kusawazisha kupitia krosi ya Juan Cuadrado.
Matokeo hayo yanaifanya Argentina kumaliza nafasi ya pili katika Kundi wakiwa na utofauti wa pointi sita, mbele yao Brazil.
Argentina watacheza na Chile wakati Colombia watamenyana na Ecuador.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares