Arsenal wamvumilie Arteta, atakuwa bora – Unai Emery

Kocha wa zamani wa Arsenal na sasa Villarreal Unai Emery amesema klabu ya Arsenal inatakiwa kuendelea kumvumilia kocha Mikel Arteta. Ameyasema hayo kuelekea mtanange wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Europa baina ya timu hizo mbili.

Emery alifutwa kazi baada ya miezi 18 pekee Novemba 2019 na kocha Arteta alichukua mikoba ya timu hiyo kwa kandarasi ya miaka mitatu.

“Wanahitaji kuwa wavumilivu, nadhani ni ndoa kamili yenye muungano mwema” alisema Emery.

“Arteta ni kocha mkubwa, unaweza ukamuona mfumo wake kiuchezaji ni wa kipekee”.

Emery, ni kocha ambaye amefanikiwa zaidi kwenye michuano ya Europa, alipata nafasi ya kukinoa kikosi cha Julai 2020, kabla ya hapo alishinda mataji matatu na Sevilla.

Mwezi Mei 2019, The Gunners walitinga fainali na kuchapwa goli 4-1 na Chelsea mchezo uliopigwa Baku.

Hata hivyo, kuelekea mtanange wa kesho Alhamis, Arsenal itakuwa bila huduma ya mshambuliaji Alexandre Lacazette ambaye ni majeruhi na Pierre-Emerick Aubameyang anasumbuliwa na Malaria.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares