Arsenal yaanza na sare ya 1-1 kwa Benfica katika mechi ya mkondo wa kwanza wa hatua ya 32 Europa League

Klabu ya Arsenal imelazimisha sare ya goli 1-1 dhidi ya Benfica katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Europa hatua ya 32 bora katika mtanange uliopigwa Rome Jana Alhamis. Mchezo huo ulichezwa kwenye dimba la Olympic na sio Ureno kutokana na vizuizi vya janga la Covid-19.

The Gunners walikuwa kwenye utawala wa mchezo kwa muda mrefu bahati mbaya kwao hawakuweza kuzitumia vyema nafasi. Goli la Benfica lilifungwa na Pizzi kwa njia ya penati kabla ya Arsenal kurudi mchezoni na kusawazisha kupitia kwa Bukayo Saka aliyemalizia krosi ya Cedric Soares.

Mkondo wa pili utachezwa wiki moja kutoka sasa, ambapo mechi hiyo itakuja baada ya mechi ngumu kwa Arsenal kwenye Ligi ya England Manchester City na Leicester City.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares