Arsenal yaanza vyema mbio za Ligi ya Europa

Arsenal imeanza vyema kampeni ya kuwania taji la Ligi ya Europa baada ya kuitandika timu iliyoonekana kuwa ngumu kwenye kundi la F ya Eintracht Frankfurt kutoka Ujerumani kwa goli 3-0.
Ulikuwa wakati wa makinda waliohitimu maisha ndani ya Emirates, Joe Willock na Bukayo Saka kwani wote wameifungia goli  moja kila mmoja na huku staa wa timu hiyo  Pierre-Emerick Aubameyang akifunga goli la 3.
Arsenal ni wanafainali wa msimu uliopita wa Europa walipofungwa na Chelsea walijikuta katika wakati mgumu kipindi cha kwanza dakika za awali kabla ya kurudi mchezoni na kushinda mtanange huo.
Kinda Willock aliitanguliza Arsenal kwa kufunga akimalizia mpira uliopoteleza uelekeo baada ya kugongwa kabla ya Saka kufunga la pili kunako dakika ya 85 dakika mbili nyingine Pierre-Emerick Aubameyang akafunga goli la 3 na kumaliza ukame wa ushindi kwenye mechi tatu mfululizo.
Kundi F litaongozwa na Arsenal wakati Standard Liege wakishika nafasi ya pili kwa alama 3 baada ya kuifunga Victoria.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends