Arsenal yabanwa 1-1 na Slavia Prague Ligi ya Europa

Kikosi cha kocha Mikel Arteta kimebanwa mbavu na kushindwa kuondoka na ushindi baada ya kutoa sare ya goli 1-1 dhidi ya Slavia Prague mchezo wa Ligi ya Europa robo fainali mkondo wa kwanza.

Ingizo jipya kutokea bechi Nicolas Pepe aliipatia timu yake ya Arsenal bao kunako dakika ya 86 lakini bao hilo lilisawazishwa dakika ya mwisho ya mchezo.

Tomas Holes alifunga goli hilo kwa Prague akifanya mchezo wa raundi ya kwanza kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mkondo wa pili ni Alhamis ijayo kuanzia saa nne za usiku.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Alexandre Lacazette pengine atalaumiwa zaidi na wenzake kufuatia kupoteza nafasi maridhawa akiwa pekee yake na mlinda mlango kabla ya kugogesha mwamba.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares