Arsenal yabanwa mbavu na Burnley

Burnley wameshindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Arsenal katika mchezo uliopigwa dimba la Turf Moor huku timu hiyo ikikosa nafasi nyingi za wazi ambazo zingeisaidia kukwea katika nafasi ya msimamo wa Ligi Kuu England, mtanange huo umeisha kwa sare tasa (0-0).

Vijana hao walionekana kama wangehitimisha ukame wa kupata ushindi mbele ya Arsenal katika michezo 11 bila ushindi lakini mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa matokeo yalikuwa suluhu.

Hendrick na James Tarkowski wangeipa uongozi Burnley kupitia mpira wa vichwa iliyokwenda nje ya lango kabla ya Jay Rodriguez kukosa nafasi ya wazi pia kwa shuti dogo alilopiga kisha kugonga mwamba.

Droo hiyo inaifanya Arsenal kufikisha alama 31 nafasi ya 10 wakati Burnley wamekamata nafasi ya 11 kwa alama 30.

Timu zote zinaingia kwenye mapumziko maalumu ambapo zitarejea dimbani Feb 15 ambapo Burnley itasafiri kuwakabili Southmpton na Arsenal Feb 16 itakuwa nyumbani kuwaalika Newcastle United.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends