Arsenal yabanwa na Watford, Everton yafundishwa Mpira na Bournemouth

Watford wamelazimisha sare ya goli 2-2 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England ambapo Arsenal ilitangulia kwa goli 2-0.
Chini ya kocha mpya Quique Sanchez Flores huo unakuwa mchezo wake wa kwanza akiwa ameingia na ushindi.
Kiungo mshambuliaji wa Watford Roberto Pereyra amefunga kwa njia ya penati katika dakika za lala salama akifanya timu hizo zigawane alama huku goli la kwanza la timu hiyo likifungwa na kiungo wa zamani wa Manchester United Thomas Williams Cleverly kunako dakika ya 53.
Strika wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang tangu atue kwa Washika mtutu hao wa London ameshathibitisha makali yake akiwe langoni kwani amefunga goli 4 kwenye mashuti 7 aliyopiga langoni mwa timu pinzani.
Bournemouth yaitwanga Everton bila huruma kwa goli 3-1 katika kile ambacho wengi hawakutegemei kutokana na usajili uliofanywa na Everton chini ya Marco Silva
Everton ambayo imekuwa na mwendo wa kuchechemea haijaanza vyema mpaka sasa kwenye michezo mitano ya awali.
Callum Wilson, Fraser wamefunga goli kwenye mchezo wa leo upande wa Bournemouth huku lile la Everton likiwekwa kimiani na Calvert-Lewin

Author: Bruce Amani

Facebook Comments