Arsenal Yabanwa Ugenini 2-2 na West Ham United
Vinara wa Ligi Kuu England Arsenal wamedondosha alama mbili kufuatia sare ya bao 2-2 dhidi ya West Ham United katika mchezo waliongoza bao mbili na kujikuta wakiondoka na alama moja dimba la London.
Gabriel Jesus na Martin Odegaard walifunga magoli ya mapema kwa Washika Mtutu wa London kabla ya kuangukia pua kwa kuruhusu hayo mabao.
Said Benrahma akafunga bao la kwanza dakika ya 33 kwa mkwaju wa penati kisha Jarrod Bowen akafunga bao la pili kipindi cha pili kwa kutumia pasi ya Thilo Kehrer.
Inakuwa sare ya pili mfululizo kwa Arsenal ambao walitoa sare ya bao 2-2 na Liverpool wiki iliyopita na kufanya sasa kuongoza msimamo wa EPL kwa tofauti ya pointi nne dhidi ya Manchester City ambao wanamchezo mmoja mkononi.
West Ham, wanaendelea kubakia nafasi ya 15 alama nne salama kutoka kwenye mstari wa kushuka daraja.
