Arsenal yachapwa 2-0 na Brentford EPL

Walipoishia ndipo wanapoanzia. Klabu ya Arsenal imeendelea kuchapwa kwenye Ligi katika msimu huu mpya, mechi ya ufunguzi baada ya kukubali kipigo cha goli 2-0 dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya Brentford mbele ya mashabiki wao.

Arsenal ambayo kwa misimu kadhaa sasa imekuwa kama pombe ya ngomani ambayo kila mmoja anajitekea mwenyewe ilianza kupokea goli la kwanza kupitia kwa Sergi Canos kabla ya Christian Noorgard kufunga la mwisho kwenye mtanange huo uliopigwa dimba la Brentford community Jana Ijumaa.

Bao la Norgaard ni la kwanza baada ya kushindwa kufunga kwenye mechi 59 za Ligi daraja la kwanza England

Jaribio haswa la Arsenal lilitokea wakati Emile Smith Rowe alipopiga shuti ambalo liliokolewa na kipa wa Brentford David Raya kabla ya Nicolas Pepe kumjaribu kipa huyo pia.

Washika Mtutu wa London walikuwa bila huduma ya nahodha Pierre-Emerick Aubameyang pamoja na strika Alexandre Lacazette. ingizo jipya Ben White kutoka Brighton alikuwa sehemu ya mchezo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends