Arsenal yaduwazwa na Sheffield United

56
Sheffield United imefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Arsenal na kupanda mpaka nafasi ya tisa kwenye msimamo wa EPL. Arsenal ikiwa imeshinda mchezo mmoja ugenini msimu huu(Newcastle United 1-0), walikubali goli la dakika ya 30 ya Lys Mousset kipindi cha kwanza kuamua mchezo.
Goli la Mousset linakuwa goli lake la kwanza msimu huu ambapo alitumia mpira wa mchezaji mwezake Jack O’Connell kuandikisha bao hilo. Swali kubwa kwa kocha Unai Emery ni kushindwa kumtumia kiungo wa Kijerumani Mesult Ozil licha ya kwamba katika eneo la kiungo la Arsenal kunaonekana kuwa na mapungufu ya ubunifu sehemu hiyo.
Ni matokeo makubwa zaidi kutokeo kwa Sheffield United tangu kupanda daraja awamu hii ambapo sasa wamekwea mpaka nafasi ya tisa wakiwa na alama 12 michezo 9. Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kupoteza nafasi ya kuingia nne bora na sasa wamesalia nafasi ya tano nyuma ya Chelsea.

Author: Bruce Amani