Arsenal yafufuka na kuichapa West Bromich Albion 6-0 Kombe la Carabao

Mshambuliaji wa kati wa kimataifa wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang amerejea uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja akijiuguza na janga la virusi vya Corona na kufunga goli tatu katika ushindi wa goli 6-0 mchezo wa Kombe la Carabao hatua ya tatu dhidi ya West Bromich Albion.

Aubameyang akicheza mchezo wa kwanza wa msimu kwa namna ya kipekee akiwa ameungana na mshambuliaji wa Kifaransa Alexandre Lacazette ambaye pia alifunga akitokea bechi.

Wachezaji wengine ambao walifunga ni winga Nicolas Pepe, na Bukayo Saka.

Ushindi huo unakuwa wa kwanza wa msimu kwa kocha Mikel Arteta ambaye alipoteza mechi mbili za Ligi za mwanzo jambo ambalo lilikuwa linaongeza hofu ya utimuliwa kwa kocha huyo.

Kiungo mshambuliaji mpya aliyekuwa anakipiga kunako klabu ya Real Madrid Martin Odegaard walikuwa kwenye ubora mkubwa kulinganisha na West Bromich Albion ambao walichezesha wachezaji watano wapya.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares