Arsenal yaichapa Man Utd ikiwa ni ushindi wa kwanza kwa Arteta

Mikel Arteta amepata ushindi wa kwanza akiwa kama Kocha mkuu wa Arsenal akiifunga Manchester United katika mtanange uliofanyika dimba la Emirates goli 2-0.

Winga na mchezaji ghali wa Arsenal Nicolas Pepe alianza kuifungia goli la kwanza kunako dakika ya nane ya mchezo akimalizia pasi kutoka kwa Sead Kolasinac na kufuta ubora wa United walioanza nao dakika za awali

Goli la pili liliwekwa kambani na mlinzi wa timu hiyo Sokratis Papastathopoulos akimalizia mpira wa kona wa Pepe baada ya makosa ya walinzi wa Manchester United

Matokeo hayo yanaifanya United kusalia nafasi ya tano, alama tano nyuma ya Chelsea iliyotoa droo na Brighton ya goli 1-1, upande wa Arsenal wamekwea mpaka nafasi ya 10 katika msimamo wa EPL.

Aidha, Arsenal wamehitimisha rekodi mbaya ya kushindwa kupata ushindi katika mechi saba waliozocheza dimba la Emirates, mchezo wa mwisho ulikuwa dhidi ya Chelsea.

Baada ya mchezo huo, Arsenal watakutana na Leeds siku ya Jumatatu huku FA, wakati Manchester United ikipepetana na Wolves hatua ya tano ya michuano hiyo.

Matokeo mengine EPL.

Southmpton 1-0 Tottenham

Manchester  City 2-1 Everton.

West Ham 4- 0 Bournemouth

Norwich 1-1 Crystal Palace

Author: Bruce Amani